WATU TAKRIBANI 600 HAWAJULIKANI WALIPO HADI SASA KATIKA MAPOROMOKO YA MATOPE NA MAFURIKO NCHINI SIERRA LEONE
Watu takribani 600 wanadaiwa kutoweka nchini Sierra Leone katika maporomoko ya matope na mafuriko yaliyotokea mapema Jumatatu hii.
Msemaji wa Rais wan chi hiyo Ernest Bai Koroma, Abdulai Baraytay ameliambia shirika la habari la BBC watu wengi wametoweka ikiwa ni takribani watu 600 katika maafa hayo yaliysababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Freetown.
“Wapendwa wengine wametoweka, takriban zaidi ya watu 600,” amesema msemaj huyo.
Wakati huo huo msamaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema umoja huo unaweka mikakati ya kuzuia magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kusababishwa na mafuriko hayo
No comments
COMMENT