"SIONI FAIDA YA VITA ILIYOPO KATI YA MAKONDA NA RUGE" -Babu Tale

Meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale ametoa dukuduku lake baada ya Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwakuanisha Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group Ruge Mutahaba kuwataka wamalize tofauti zao.
Tale kupitia mtandao wa Instagram, ameandika kuonyesha amefurahishwa na hatua hiyo iliyofanyika Mkoani Tanga katika uzinduzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta.
“Kama kuna vita ilikua inanikera ni vita hii mmoja Mlezi mwingine mdau mkubwa kwenye kazi yetu basi hata aujui lakufanya mwisho wasiku unaishi kuumia kinyemela. Haya mzee kasema kashikaneni mikono hii inamaana mje tuijenge Dar.”-Alisema Babu Tale

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.