HII NDIYO HISTORIA NZIMA YA MAISHA YA ROMA MKATOLIKI
Ikiwa ni siku chache toka Roma Mkatoliki aachie wimbo wake mpya ‘Zimbabwe’ ambao unafanya vizuri kila kona, Alhamisi hii rapa huyo ametoa kauli yake ya kwanza Instagram ikielezea historia ya maisha yake aliyoipa jina ‘A_Journey_To_Zimbabwe’.
Rapa huyo ametoa ujumbe huo ukiwa ni ujumbe wa kwanza kupitia akaunti hiyo ya Instagram iliyoachiwa hivi karibuni kutoka kwa watu waliokaiteka.
Katika taarifa yake hiyo Roma amedai hiyo ni sehemu ya kwanza bado ataendelea kutoa taarifa mpya kupitia ukurasa huyo.
Ujumbe wa Roma
#Sehemu_Ya_1
Ilikuwa Ni Usiku Majira Ya Saa Saba Kasoro, hali ya hewa ikiwa ni ya ubaridi kutokana na Mvua zilizokuwa zinanyesha Kipindi hicho, zilizoambatana na upepo mkali uliokuwa unavuma pembezoni mwa Bahari,Ilisikika Sauti Ya Mtoto Mchanga akilia saanaa Katika Moja Ya wodi ya Hospitali fulani Iliyokuwa Imejengwa Pembezoni mwa Bahari Hiyo.Nilihadithiwa kuwa ilikuwa ni siku ya Ijumaa Ya Tarehe 12 mwezi wa 12 miaka ya 80 naa(Takribani Miaka zaidi ya 30 sasa imepita), Katika Hospitali Ya Bombo Mkoani Tanga (Mjini), sauti hiyo ya kichanga kilichokuwa kinalia ilikuwa ni ishara kuwa ulimwengu umeongeza kiumbe mwingine katika Ardhi Ya Tanzania Barani Afrika.Alionekana Mwanamke Amejilaza kitandani akiwa amechoka huku pembeni yake kikiwepo kichanga hicho chenye Kg 3.5 Na afya Njema Bila Kasoro yoyote, Kikinyonya Ziwa la kuume la mama huyo, hakika ilikuwa ni furaha kwa familia hii.Furaha iliongezeka zaidi pale ilipofika muda wa kuona wagonjwa ambapo familia yote akiwemo baba wa kichanga hiki alikuja kumuona kidume wake, na jambo lililofurahisha zaidi ni kuwa kila mtu katika familia (kaka/dada/mamdogo) alikuwa ana jina lake kichwani alilopanga kumpatia kichanga hiki,wakati huo huo mama mzazi yeye alishapanga jina lake la kumpa mwanae, Ndipo mabishano yalipoanza wodini hapo kila mtu akisema aitwe flani aitwe flani aitwe flani….kelele hizo zilipelekea Nurse wa zamu awatoe Nje Kwa sababu ilikuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wengine,ikawa hivyo siku ikaisha kichanga hicho hakijapatiwa jina.Baada ya muda mama na mwanae walipata ruhusa kurudi nyumbani na ukawa mwanzo wa maisha mapya katika familia hii.Lakini Siku tu mama huyu alipokifukia tu kitovu cha mwanae na kumpa jina #Ibrahimhuku baba mtu akikataa na akitaka mtoto aitwe #Ismail au #Isihaka na ndugu wengine walitaka mtoto aitwe #Idrissandipo visa/mikasa/misukosuko ilipoanza kuiandama familia hii…..
No comments
COMMENT