SHAMSA FORD APOKEA NGUMI YA USO KATIKA HARAKATI ZA KUAMLIA UGOMVI

Msanii wa filamu Shamsa Ford amepokea kichapo Jumanne hii katika harakati za kuamlia ugomvi wa watu ambao haijajulikana moja kwa moja ni nani, na sababu za ugomvi wao ni nini.

Malkia huyo wa filamu amekutwa na mkasa huo ikiwa ni mwezi mmoja toka aibiwe akaunti yake ya Instagram yenye followers zaidi ya milioni 2.
Muigizaji huyo amedai alipigwa ngumi ya uso katika harakati za kutafuta usalama wa watu hao ambao walikuwa wakipigana.
“Jana kwa moyo mmoja nimeenda kuamlia ugomvi watu wasipigane mwisho wa siku nikaambulia Mimi ngumi..HUYU mtu alishiba sana aiseee ngumi ilikuwa nzito sana.. niombeeni ndugu zangu panauma,” aliandika Shamsa Instagram.
Kwa sasa muigizaji anaendelea na matibabu

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.