MAHASIMU WA JIJI MOJA WATINGA NUSU FAINAL KATIKA MICHUANO YA UEFA

Ligi ya klabu bingwa Ulaya msimu huu imefikia kikomo baada ya klabu ya Leicester City ya Uingereza kutoka sare na Atletico Madrid uwanjani King Power.

Leicester wameondolewa katika hatua ya robo fainali baada ya sare hiyo ya 1-1 huku wakiwa wamefungwa 1-0 kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.
Mchezaji wa Atletico Madrid, Saul Niguez alifunga bao kwa kichwa dakika ya 26.
Hii lilikuwa na maana kwamba walihitaji mabao matatu kipindi cha pili ili kufanikiwa kusonga.
Jamie Vardy alikomboa bao moja dakika ya 61 lakini Atletico walifanikiwa kujilinda hadi dakika ya mwisho na kuhakikisha wanajiunga na Real Madrid kwenye nusu fainali.

Real waliwalaza Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao 4-2 na kupata ushindi wa jumla wa 6-3, ambako katika mchezo wa kwanza uliochezwa Ujerumani, Real Madrid walishinda kwa goli 2-1, baada ya kupata ushindi ambao ulipatikana ndani ya dakika 120.
Cristiano Ronaldo alikuwa mchezaji hodari wa mechi na kuleta madhara makubwa kwa kufunga hat-trick katika game hiyo. Matokeo hayo yanaifanya Real Madrid na Atletico Madrid, kufuzu hatua ya nusu fainali

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.