SIMBWA YAENDELEA KUBAKI NA POINTI TATU ILIYOPEWA NA KAMATI YA MASAA 72
Kamati ya katiba, Sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) limemaliza kikao chake na klabu ya Simba usiku wa kuamkia leo na kuazimia Simba inaendelea kubaki na pointi ilizopewa na Kagera Sugar.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuahirisha kikao.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena na pamoja na mashahidi wengine kuhojiwa. “Kuna watu wanatakiwa kuhojiwa, na kamati itakaa wiki hii. Tunawatafuta wahusika na wakipatikana tu, itapangwa siku. Baada ya hapo kamati itatoa maamuzi,” alisema Mwesigwa.
Kikao hicho kilifanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa simba, Kagera Sugar, na waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa.
Kabla, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Kamati hiyo ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi tatu za njano.
Lakini Kagera Sugar wakaendelea kusisitiza kwamba Fakhi alikuwa na kadi mbili tu za njano alizopewa katika mechi ya Mbeya City na ile dhidi ya Majimaji na si dhidi ya African Lyon, huku mchezaji Venance Ludovic ameidhinishwa kuwa mchezaji halali wa African Lyon.
Katiba, Sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) imepitisha uamuzi huo katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Timu ya African Lyon imepigwa faini ya Sh 500,000 kutokana na kuonekana kuwa hawakufuata utaratibu katika usajili wake.
Mchezaji huyo alikuwa akilalamikiwa kwamba hakukamilisha usajili wakati anajiunga Lyon akitokea Mbao FC
No comments
COMMENT