LINGARD APEWA MKATABA MPYA NA UNITED

Mchezaji wa Manchester United Jesse Lingard amesaini mkataba mpya na timu yake na atakua akilipwa mshahara wa paundi 75,000 kwa wiki na kama timu yake watafuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya atapata paundi 100,000 kwa Wiki.

Mkataba wake huo mpya utabakisha Jesse klabuni hapo mpaka mwaka 2021 na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka moja zaidi katika mkataba huo wa sasa.
Lingard ameichezea klabu yake jumla ya michezo sabini, msimu huu amecheza michezo 29 na kufunga mabao 5 na alijiunga ma timu hiyo akiwa na umri wa miaka saba.
Mchezaji huyo alianza kuchomoza chini ya meneja Louis van Gaal na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo kwenye Klabu za Leicester City, Birmingham City, Brighton na Derby County

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.