ROMA ARUDI KWA HOFU TANZANIA HUKU AKIAMUA KUJITOA MUANGA KUELEZEA JIMBO YAKE MPYA YA ZIMBAMBWE
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki amewasili jana usiku akitokea nchini Zimbabwe alikoenda kikazi.
Roma Mkatoliki ambaye ameachia wimbo wake mpya wa Zimbabwe wiki iliyopita amejikuta akisakwa na vyombo vya habari kuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo lakini hakuwepo nchini na kumuachia jukumu hilo la kutambulisha wimbo huo kwenye Media, mke wake.
“Kiukweli nimechoka wanangu what i need ni kuona familia yangu, mke wangu na mtoto na ndugu, jamaa na marafiki”,amesema Roma Mkatoliki jana usiku alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, jijini Dar es salaam.
Alipoulizwa ni kwanini alimtuma mke wake aachie wimbo huo ile hali alikuwa nje ya nchi Roma Mkatoliki amesema alifanya hivyo kwa sababu muda ulifika wa kutoa ngoma hiyo na tayari alifanya booking na Media, lakini alikataa kuzungumzia wimbo huo wala kueleza alichoenda kufanya Zimbabwe huku akiahidi mashabiki wake kuwa kuanzia leo ataanza Media Tour kuuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo .
Wakazi, Stamina, Ndugu jamaa na Marafiki zake wa karibu wa Roma walikuwepo kwenye mapokezi hayo ambayo yalikuwa kimya kimya.
No comments
COMMENT