BARCELONA WAMTOA KAFARA RACTIC ILI WAMPATE COUTINHO
Klabu ya soka ya Barcelona bado inaendelea kupambana kumtafuta mbadala wa Neymar Dos Santos na wanamuona Phellipe Coutinho kama mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Neymar.
Coutinho mwenyewe anaonekana anataka kwenda Barcelona na inadaiwa ameomba kuuzwa lakini klabu ya Liverpool bado inamuwekea ngumu kiungo huyo kuondoka.
Liverpool walishakataa ofa mbili za Barcelona ambapo moja ilikuwa ya £80m na nyingine ilikuwa ya £90m na kusisitiza kwamba kiungo huyo haondoki klabuni hapo kwa dau lolote lile.
Sasa Barcelona wamekuja tena na safari hii wamekuja na mchezaji pamoja na pesa, ni Ivan Ractic kiungo kisheti wa Barca ambaye wako tayari kuwapa Liverpool na kiasi cha pesa ili kumchukua Coutinho.
Nchini Uingereza mashabiki wengi wa Liverpool wanaonekana kutoridhishwa na jambo hili huku wengine wakisema ni sawa na kupewa mguu mmoja na kukatwa mwingine.
Coutinho hakuwepo jana kwenye safari ya Liverpool nchini Ujerumani ambapo Liverpool walikwenda kucheza dhidi ya Hoffeinman lakini sababu ya kutokuwepo kwenye safari hiyo ikitajwa kuwa ni majeruhi.
Tazama VIDEO
No comments
COMMENT