NEYMAR AKUBALI KUWA BAROZI WA WATU WANAO ISHI KWENYE SHIDA
Nyota mpya wa PSG, Neymar amekubali kuwa balozi wa watu wanaoishi kwenye matatizo kupitia tasisi ya Handicap International.
Handicap International imekuwa ikiwasaidia watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani, hasa wale wanaoshi katika maisha magumu.
Kazi kubwa ya taasisi hiyo ni kuonyesha watu hao pamoja na kuwa na shida inayozaa maisha magumu lakini wanastahili kuishi kwa usawa kama wanadamu wengine.
Neymar sasa ni mchezaji wa PSG aliyojiunga nayo akitokea Barcelona na kuweka rekodi ya day la usajili la pauni million 198.
Neymar ametangazwa kuwa balozi wa taasisi hiyo na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na jana alitangazwa rasmi jijini Geniva, Uswiss.
Wakati Neymar akitangazwa, baba yake mzazi Neymar Santos Senior na mkewe ambaye ni mama mzazi wa Neymar, Nadine Santos, pia walikuwepo.
No comments
COMMENT