CHID BENZI NDO BASI TENA MADAWA YA KULEVYA YANAZIDI MMALIZA AKAMATWA NA POLISI TENA
Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema Chid Benz amekamatwa na watuhumiwa wengine saba kufuatia msako mkali uliofanyika August 12 majira ya jioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema Chid Benz amekamatwa na watuhumiwa wengine saba kufuatia msako mkali uliofanyika August 12 majira ya jioni.
“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema.
Chid Benz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Muda’ aliyomshirikisha Q Chillah si mara ya kwanza kukutwa na tuhuma kama hizo kwani alishawahi kukamatwa na dawa za kulevya aina bangi mkoani Mbeya
No comments
COMMENT