RATIBA YA LIGI KUU BARA MSIMU MPYA 2017/18 YAWEKWA WAZI RASMI

Pazia la Ligi Kuu soka Tanzania Bara linatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi hii leo kwa timu mbali mbali kuingia uwanjani na kuanza kwa michuano hiyo mikubwa kabisa hapa nchini.

Msimu huo mpya wa Vpl wa mwaka 2017/2018 wenye jumla ya timu 16 unaanza kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti.
Mabingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Ngao ya Jamii, Simba SC leo itatupa karata yake ya kwanza kwa kuwavaa Ruvu Shooting, wakati michezo mingine itakayo pigwa ni Ndanda FC dhidi Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, huku Mwadui FC ikikipiga na Singida United.
Michezo mingine ni Mtibwa Sugar itakayocheza na Stand United, Kagera Sugar dhidi ya Mbao FC, Njombe Mji FC ikitarajia kutupa karata yake ya kwanza kunako Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons wakati mchezo wa mwisho ni vijana wa Manispaa ya Mbeya timu ya Mbeya City ikiingia dimbani kukipiga dhidi ya Majimaji FC ya Songea.
Wakati Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Dar es salaam Young Africans ikatarajia kuingia uwanjani hapo kesho  Agosti 27 mwaka huu kumenyana na Lipuli FC.TIB

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.