MAMA ASHURA AMPONGEZA ALIKIBA BAADA YA -SEDUCE ME

Mchekeshaji kutoka Timau Entertement, Mama Ashura amelipuka kwa kumsifia Alikiba baada ya hapo jana kuachia ngoma yake mpya ya ‘Seduce Me’.

Kupitia mtandao wa Instagrama muigizaji huyo ameandika ”
#Kiba umetoa wimbo mzuri japo umewasubirisha mno! Ninaimani wimbo huu utapendwa na wengi!
MAONI YANGU!
Kwa style ya wimbo yenyewe na midundo yake nilitaraji kuona dance ya kufa MTU! Hii ndio kasoro pekee ninayoiona kwenye #SeduceMe,(Kwamtazamo wangu) wimbo kama huu inatakiwa uache dancing style mtaani ambayo itakumbukwa wakati wote!
Sijajua kwanini umeamua kufanya video ya kujibana bana! Je Muda wa kuandaa kwa ukubwa zaidi ulikosekana?? Au bajeti??? Ila naamini uwezo wa pesa unao na muda unao kilichokosekana hapo ni ubunifu zaidi!
Pata picha kwa midundo hii alafu kungekua na madancer wamevaa vizuri wamependeza wanadance step zuri za level za kimataifa, locations zuri zilizoandaliwa vizuri. Aisee hii ngoma ingetusua zaidi!
NASHAURI kiba utoe REMIX ya video ili ngoma ifikie 100% na uweke ma dance ya maana sio kwenye location moja, model kwenye video mmoja dah hii inakua haina tofauti na Aje Remix!
NI MTAZAMO WANGU TUU
👌👌@malkia_wauswazi.”
Kwa miezi iliyopita msanii huyo alituhumiwa na mashabiki kuwa amemponda mkali huyo kwa kumwambia anamtegemea Diamond ili aweze kuishi katika muziki, baada ya kufanya naye mahojianao maalumu kupitia Bongo5, Mama Ashura alisemea kuwa aliongea vile hakuwa na maana mbaya bali aliongea kutoa ushauri tu.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.