RONALDO ATARAJIA KUPATA WATOTO MAPACHA HIVI KARIBUNI
Imeripotiwa kuwa kuna taarifa za mchezaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo anataraji kupata mapacha wawili wakiume hivi karibuni kutoka kwa mwanamke ambaye amempa mimba (A Surrogate Mother) huko pwani ya magharibi nchini Marekani.
Mchezaji huyo amewaambia wanafamilia yake kuwa mapacha hao baada ya kuzaliwa watasafirishwa mpaka kwenye Mansion yake yenye thamani ya pauni milioni 5 iliyopo huko mjini Madrid,Hispania.
Chanzo kimoja kinasema kuwa Ronaldo na familia yake wanahamu ya kuwaona memba hao wapya katika ukoo wao.
“Anapenda kutoweka uwazi katika maisha yake binafsi lakini amewaambia watu anaowapenda na marafiki wa karibu kuwa watoto hao wanataraji kuwasili hivi karibuni”.
Mreno huyo ambaye ana miaka 32, mpaka sasa hajawahi kumuweka wazi mama wa mtoto wake wa kwanza Cristiano Jr ambaye amezaliwa mwaka 2010.
Ripoti zingine zinadai mama wa mapacha hao ni Gergina mpenzi wa sasa wa Ronaldo. Lakini Georgina anaonekana yupo busy na Instagram na picha anazopost zinaonesha kabisa hana mimba. Miezi michache iliyopita Georgina alionekana hadharani na Cristiano Ronaldo lakini hakuwa na dalili yoyote ya mimba.
Ronaldo ambaye amefunga Magoli 18 Mpaka sasa katika ligi kuu Nchini Hispania msimu huu
No comments
COMMENT