MAREKANI YAISHAMBULIA SRIYA KWA MABOMU
Marekani imefanya shambulizi la makombora takriban 50 ,yalipigwa katika kambi ya jeshi la anga mjini Homs nchini Syria.
Awali maafisa wa Marekani walisema wana mpango wa kuchukua hatua za kijeshi baada ya Syria kushutumiwa kutumia silaha za kemikali katika mji unaodhibitiwa na waasi, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha.
Mashambulizi hayo yametekelezwa kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameamuru kutekelezwa kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria huku akitoa wito kwa mataifa yote yaliyostaarabika kukomesha vitendo vya mauaji na umwagaji damu nchini humo
Naye mshirika wa Syria Urusi ametahadharisha madhara yatokanayo na hatua zozote za kijeshi zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Syria .
Hata hivyo Rais Donald Trump amsema kuwa ,kutumia gesi hatari kuua raia wakiwemo watoto wengi, utawala wa Syria ulikuwa umevuka mipaka
Mike Pregent ni mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati ameiambia BBC kuwa mashambulizi hayo yametoa ujumbe mzito kwa Assad.
Shambulio hilo linawapa Watu wa Syria matumain, na ninachomaanisha ni kuwa haya hakika haya ni Mashambulizi dhidi ya vikosi vya anga vya Assad, silaha za kemikali, pengine dhidi ya hifadhi za mafuta halikadhalika.hivyo haikuwa dhidi ya raia, haikuwaweka marubani wa kimarekani hatarini. Ulikuwa ujumbe maalum kwa Assad kuwa usitumie jeshi lako la anga kuwaadhibu raia, hivyo nafikiri ni ujumbe wenye nguvu
No comments
COMMENT