WANAUME NANE WAKAMATWA NCHINI UGIRIKI
Ugiriki inasema imewakamata wanaume wanane, ambao wamewasili nchini humo kwa helikopta ya jeshi la Uturuki.
Helikopta hiyo ilitua mji wa Alexandroupolis, kaskazini mwa nchi, muda mfupi uliopita.
Vyombo vya habari vya Ugiriki vinasema wanaume hao wameomba hifadhi ya kisiasa.
Hii inajiri baada ya wanajeshi waasi nchini Uturuki, kujaribu kuipindua serikali katika jaribio lililofeli.
No comments
COMMENT