PASI YA KUSAFIRIA YA AU YATARAJIWA KUANZISHWA
Mkutano wa mataifa ya muungano wa Afrika unaoendelea huko Kigali Rwanda unatarajwa kujadili kwa kina swala la mizozo ya Burundi na Sudan kusini miongoni mwa mengineyo.
Pia wanatarajiwa kuanzisha pasi ya kusafiria ya AU. Lengo la pasi hiyo ni kurahisisha usafiri wa waafrika ndani ya bara lao na vile vile kuendeleza biashara miongoni mwa mataifa ya kiafrika.
Passport hiya kwanza itapewa viongozi wa mataifa ya kiafrika na maafisa wa ngazi ya juu katika AU, na baada ya miaka miwili itaweza kutolewa kwa raia wa kiafrika wataokaotoa maombi .
Pia kikao hicho kinatarajiwa kumteua mwenyekiti mpya kwani Bi Nkosazana Dlamini-Zuma anaachia usukani baada ya mda wake wa kuhudumu kukamilika
No comments
COMMENT