WANAJESHI WA UTURUKI 104 WAMEUWAWA BAADA YA KUSHINDWA KUMPINDUA RAIS WA NCHI IYO
Naibu mkuu wa jeshi la Uturuki ametangaza kwa njia ya runinga kuwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi limeshindwa.
Jenerali Umit Dundar alisema kuwa wapanga mapinduzi 104 wameuauwa. Pia amesema kuwa watu wengine 90 wakiwemo polisi na raia wameuawa.
Usiku kucha miji ya Ankara na Istanbul ilikumbwa na milio ya risasi na milipuko baada ya wanajeshi waasi kufanya mashambulizi wakitumia vifaru na helikopta.
Maafisa wanasema kuwa zaidi ya wanajeshi 1500 wamekamatwa huku wale wa vyeo vya juu wakiwemo majerali wakipokonywa nyadhifa zao
No comments
COMMENT