MTOTO WA OSAMA AAPA KULIPIZA KISASI CHA BABA YAKE

Image copyrightGETTY
Image captionKiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden
Mwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.
Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika mitandao Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa Marekani kwa kumuua babake 2011 huko Pakistan.
Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa alikuwa na babake makomando wa Marekani walipowavamia na kumtwaa ameapa kuendeleza kazi aliyoianza babake.
Image copyrightFLAGG MILLER
Image captionUjumbe huo ni wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama,"
''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia '' shirika la habari la Reuters linamnukuu.
''na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osma ole wenu, kwanini sisi tutakuwa tukilinda dinia ya kiislamu'' alisema Hamza.
Image captionnyumba alikopatikana Osama bin Laden mwaka wa 2011 huko Pakistan
Osama aliuawa na makomando wa marekani katika maficho yake huko Pakistan mwaka wa 2011.
Hamza ambaye kwa sasa ana umri wa kati ya miaka ishirini hivi alikuwa na babake kabla ya mashambulizi ya kigaidi ya mwaka wa 9/2001 huko Afghanistan kabla ya kukimbilia Pakistan kufuatia mashambulizi makali ya Marekani na washirika wake.
Hamza kulingana na wachanganuzi anatambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi hilo Ayman al-Zawahiri katika ujumbe huo unaolenga kuwavutia vijana ambao kwa sasa wamejiunga kwa wingi na kundi la Islamic state.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.