WIMBO MPYA WA JUSTIN BIBER AKIMSHIRIKISHA SERENA GOMEZ YATOKA
Kila baada ya wiki mbili, Drake anazindua kazi mpya za wasanii mbalimbali kupitia radio yake ya OVO Sound Radio kupita Beats 1 ya Dr. Dre… kwenye episode mpya ya radio hiyo producer mwenye jina ‘Nineteen85’ alivujisha collabo mpya ya Justin Bieber na mpenzi wake wa zamani Selena Gomez.
Japo wawili hao sio wapenzi tena, waliamua kuungana kwa ajili ya kutengeneza single mpya iliyopewa jina ‘Strong’ , wimbo ambao kwa namna moja ama nyingine umegusa uhusiano wao wa zamani.
Haijajulikana kama collabo hii itapatikana kwenye Album mpya ya Justin Bieber‘Purpose’ inayotegemea kuwa hewani November 13 mwaka huu 2015 lakini tutegemee collabo nyingine kwenye Album hiyo na wasanii kama Nas, Travis Scott, Big Sean, Ed Sheeran na Ariana Grand
No comments
COMMENT