MTANDAO UNAO SAMBAZA MKANDA WA LIL WAYNE WAPO MATATANI,WANASHERIA WATAKA KUCHUKUA HATUA
Wiki kadhaa zilizopita tulisikia kuwa kuna mtu anashikilia mkanda wa utupu wa Lil Waynena amekusudia kuusambaza kwenye blogs na websites mbalimbali zinazopokea mikanda hiyo, wanasheria wa Lil Wayne wakasema itakuwa ngumu kwa yoyote kuuza mkanda huo bila idhini ya rapper mwenyewe, na kama ikitokea hivyo basi watachukua hatua kali dhidi ya mtandao huo… kuna mabadiliko yoyote?
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, mkanda wa utupu wa rapper Lil Wayne umeweka headlines kubwa sana baada ya mtandao wa HollywoodStreetKing kuanza kuachia vipande vya mkanda huo na kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, inaonekana Lil Wayneameanza kukerwa na kitendo hiki.
Wanasheria wa Lil Wayne wameamua kuchukua hatua dhidi ya blog yaHollywoodStreetKing, kwa kuandika barua inayowaonya mtandao huo kuhusu kutumia video hiyo…
>>> “Mteja wetu anawataka muache kutumia videos mnazoziweka kwenye mtandano wenu mara moja, muache kusambaza nakala zozote za video hiyo, ikiwemo nakala za kielektroniki, pia mzifute nakala zozote zilizopo ili kutoendelea kuvunja haki zozote alizonazo mteja wetu Mr. Carter…” <<< ilisema moja ya sehemu ya barua hiyo.
No comments
COMMENT