T.I ALISEMA HAWEZI KUMCHAGUA RAIS MWANAMKE ,KANYEWEST PAMOJA NA J Z WANASEMAJE WAO
Baada ya kutangaza nia yake ya kugombea Urais wa Marekani kufikia mwaka 2020,Kanye West amekuwa akiweka headlines nyingi zinazohusiana na viongozi wa Siasa.
Licha ya rapper T.I kuonyesha wazi kuwa hatotoa kura yake ya Urais kwa mwanamke,Hillary Clinton ambaye pia ni mgombea Urais, Kanye West ameonekana kuwa na nia tofauti kabisa… kwa mujibu wa mtandao wa Buzzfeed, rapper na producer Kanye Westameamua kuweka nguvu zake kwa mgombea huyo na kuamua kuchangia pesa za kuendesha kampeni za mgombea Urais, Hillary Clinton anaegombea Urais kupitia Chama cha Democratic Party, alichopo Rais Barrack Obama.
Japo mtandao wa Buzzfeed, haujaweka wazi ni kiasi gani cha pesa ambacho Kanye West kaamua kutoa kwenye kamati ya Mama Hillary, Kanye sio msanii wa kwanza waHipHop kutoa support hiyo kwa mama huyo… rapper Ja Rule pia hivi karibuni alisikika akisema kuwa support yake kubwa ameiweka kwa mgombea huyo zaidi.
Jay Z pia ameonekana akishirikiana na kamati ya kampeni ya Hillary Clinton kwa ukaribu sana, huku kamati hiyo ilitumia zaidi ya dola 15, 000 ambayo ni sawa na milion 34 za Kitanzania kwenye restaurant ya Jay Z ’40/40′ kwa ajili ya catering, chakula na vinywaji mwezi uliopita.
Wasanii wengine wanaomuunga mkono Mama Hillary Clinton ni Jessica Alba, Matt Damon na Tom Hanks ambao wote pia tunaambiwa wamechangia kwa namna moja ama nyingine kugharamia kampeni za Mama Hillary Clinton.
No comments
COMMENT