MSANII LINAH SANGA ADAI PENZI LAKE NA MGANDA KAKA YAKE ZARI LIPO IMARA
Hitmaker wa Ole Temba, Linah Sanga amesema uhusiano wake na raia wa Uganda, Williams Bugeme ni imara zaidi ya vile wengi wanavyodhani.
Linah ameiambia Bongo5 kuwa uvumi kuwa tayari wameachana na mpenzi wake huyo, umetokana na kuonekana kutokuwa naye karibu kama zamani.
“Mimi nashangaa watu wanataka nini?” amehoji. “Watu wanafikiri mimi na mpenzi wangu tunaweza kuachana kirahisi! Sisi tunapendana kweli. Sema sasa hivi tumeamua kuacha kuweka picha zetu mara kwa mara kwenye mitandao, ila sisi tupo poa na kila mtu anaendelea vizuri.”

No comments
COMMENT