MASHABIKI WA MAN U WAMKOMALIA BOLT BAADA YA KUIBUKA NA JEZI YA ARSENAL
Mwanariadha nyota duniani, Usain Bolt anajulikana ni shabiki damu wa Manchester United.
Unakumbuka amekuwa akihudhuria hadi mazoezi ya timu hiyo tokea enzi za Alex Ferguson.
Lakini juzi ameonekana akiwa ameng’ara katika uzi wa Arsenal, jambo ambalo limewaudhi baadhi ya mashabiki wa Arsenal.
Mashabiki wengi wamekuwa wakitupa lawama zao kwa Bolt kupitia mitandao mbalimbali kwamba haeleweki.
Tena lawama zinakuwa kali zaidi kwa kuwa wiki iliyopita, Arsenal ilikutana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Arsenal.
Lakini taarifa zinaeleza, Bolt alikuwa kazini kwa kuwa anadhaminiwa na Puma kama ilivyo kwa Arsenal.
No comments
COMMENT