MANENO YAKE MINAJ KUHUSU DRAKE NA MIK MILL $BIFU LAKE NA MILEY CYRUS


First lady wa label ya Cash Money Records Nicki Minaj ameingia kwenye headlines za burudani baada ya interview yake na jarida la The New York Times Magazine, miongoni mwa majarida makubwa ya mastaa wa kike wa HipHop Marekani.
MINAJESTY3
Akiwa kwenye interview na jarida hilo Nicki Minaj alizungumzia vitu vingi baadhi vikiwa mtazamo wake kuhusu beef ya Drake na mpenzi wake Meek Mill pamoja na beef yake na Miley Cyrus msanii wa Pop nchini Marekani... kwenye mazugumzo Nicki alikuwa na haya yakusema kuhusu Miley Cyrus..
>>> ” kitendo cha yeye kukasirishwa na nilichokisema kuhusu kitu kinachowagusa wanawake weusi kinanifanya nimchukulie tofauti. Yeye kila siku yupo kwenye videos na watu weusi haswa wanaume na mara nyingi anawaaakila wasanii wa weusi wa kike kwenye majukwa yake tofauti, lakini eti hutaki kujua wanawake weusi wanajisikia vipi kuhusu vitu muhimu vinavywagusa (kama ile tuzo)!? Sio kweli, huwezi kutaka mazuri tu kuhusu sisi bila kupenda au kuelewa mabaya yanayotuzunguka. kama anapenda kuenjoy lifestyle yetu na kuwa karibu na sisi, kuimba na kuperform na sisi basi inabidi ajue yale mambo yanayotugusa na kutuumiza pia, na sio tofauti!” <<< Nicki Minaj.
MINAJESTY2
Nicki Minaj: (NY Times Magazine Photo Shoot)
Na alipoulizwa kuhusu beef ya Meek Mill na DrakeNicki Minaj alikuwa na haya ya kusema…
>>> “Wale ni watu wazima, watu wazima wenye akili zao timamu… hii issue ni kati yao wawili wao ndio wanajua wanaipeleka wapi hii beef… ila binafsi siipendi, sijiskii vizuri kuwaona wakiwa hivyo, na siku zote maamuzi ya busara ni kutokuchagua upande haswa issue ikiwa inawahusu watu wawili unaowapenda. Kwanza ni ujinga. Nataka tu yaishe soon.” <<< Nicki Minaj.
MINAJESTY4
Badaae Nicki Minaj akaulizwa kuhusu baba yake aliewakimbia na kama amechangia kwa kiasi kikubwa kwa yeye kuwa na ubabe alionao leo, Nicki alijibu hivi…
>>> “Yule alikuwa katili sana. Kwanza mara nyingi nilikuwa namsikia anagomba na kutukana sana, mara nyingi! Na hiyo ilinifanya nikue nikijua hiyo ndio namna ya kuishi, kwa sababu ndivyo nilivyokuwa nikikua na kumuona anaishi!” <<<Nicki Minaj.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.