HATIMAYE FROLA MBASHA AMPIGIA MAGOTI MUMEWE AOMBA AMSAMEHE

Ule usemi wa Mwanaume ni Mwanaume tu, Umetimia leo baada ya Makeke yote na Mbwembwe zote za Flora Mbasha Kumuishia na Kujikuta amekua mdogo kama piriton mbele ya Mumewe.

Nikakumbuka ule usemi wa Baba na Mama wakigombana Nyumbani, Waache wenyewe Mwisho wataelewana.

Wakati alipokua anahojiwa na Millad Ayo, Flora Mbasha kasema; "Yule ni mume wangu na bado nampenda na ntaendelea kumpenda. Tuna watoto wawili na ningependa tuongeze watoto mapacha lakini tusubili uchaguzi Uishe. Nlikua nampenda mume wangu sana ndo maana pete naivaa shingoni hii ndoa yangu na Mume wangu naipenda sana. Naomba anisamehe kwani nmeshamsamehe pia

Nipo na amani tele na namshukuru Mungu.

Namuahidi ntaendelea kumpenda siku zote. Ninachomuomba naye anisamehe" amesema Flora.

Mbasha mwenyewe kasema Kibiblia hakuna kuachana. Alikua natuma watu wamuombee Msamaha ili Flora arudi nyumbani walee watoto.

"Asisikilize watu na watu wanaompamba, Naomba arudi nyumbani" alinukuliwa Mbasha.


Lakini Baada ya mke wake kufuta kesi mahakamani na kufuta kesi ya kudai talaka, na Kumpigia Magoti Mumewe, Mume amegoma tena, amesema hamuhitaji tena. Kabadilisha maamuzi.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.