KIIZA AZAWADIWA TUZO NYINGINE

Baada ya klabu yake ya Simba kumtangaza kuwa mchezaji bora wa mwezi September siku kadhaa zilizopita Hamis Kiiza ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo nyingine tena.Kiiza ambaye awali kulikuwa na stori kuwa Simba wanataka kumtema kutokana na kutofanya vizuri katika mechi za maandalizi ya msimu, ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika Ligi Kuu Tanzania bara.
DSC_00212 (1)
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda ametwaa tuzo hiyo ambayo alikuwa akiwania na Elias Maguli wa klabu ya Stand United ya Shinyanga na Amissi Tambwe ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayeichezea klabu ya Dar Es Salaam Young African.

Kiiza atazawadiwa Tsh milioni moja kutoka katika kampuni ya mawasiliano ya simu za mkono ya Vodacom ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Tanzania bara. Katika mechi za mwezi September Kiiza alifanya vizuri kwa kufunga hat-trick katika mechi dhidi yaKagera Sugar lakini katika mechi tano walizocheza mwezi September Kiiza amefunga jumla ya magoli matan

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.