GOOD NEWS VIDEO YA SUGUA GAGA YA SHAA YA FIKIA IDADI HII YA WATAZAMAJI

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Shaa anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani! Tarehe 22 February mwaka 2014 msanii huyo wa Bongo Fleva aliachia single yake ya ‘Sugua gaga’ video ambayo ilifanya vizuri na kupendwa sana na mashabiki wa hapa nyumbani… lakini hii ikoje kwa watu wetu nje ya Tanzania?
Ukitembelea YouTUBE muda huu utagundua kitu tofauti kwenye idadi ya watazmaji wa video ya Shaa ‘Sugua gaga’, ukiipitia channel ya Muziki kwenye YouTUBE utagundua kuwa watazamaji wa video hiyo wamefika milion 1,337,621
shaa3
Lakini good news ni kwamba, ukitembelea tena YouTUBE channel ya mtu anayejiita‘Seka Moke’ utagundua utofauti wa idadi ya watazmaji mtu wangu, kupitia channel hiyo, video ya ‘Sugua gaga’ imetazamwa na watu milion 20,311,512′ tofauti ya watazamaji zaidi ya milion 18 kwenye channel ya Muziki!
shaa2
Hiki ni kitu kizuri sana, kwani kama unakumbuka hapo awali video ya ‘Number One Remix’ ya Diamond feat Davido iliingia kwenye headlines baada ya kufikisha idadi ya watazamaji milion 10, 897, 186 lakini time hii ni zamu ya Shaa kuipeperusha bendera yaTanzania kwa kuwa na watazamji wengi zaidi kwenye wimbo mmoja!
Big up sana Shaa!
Unaweza pia ukaicheki video ya Shaa ‘Sugua gaga’ hapa chini mtu wangu.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.