BLATTER NA MICHEL PLATIN WASIMAMISHWA NA KAMATI YA MAADILI FIFA KWA KOSA LA UFISADI
Sakata kubwa linalowakabili wawili hao ni kutumia kwa kiasi kibubwa cha fedha kutoka kwenye account ya FIFA na kuingia moja kwa moja kwenye account ya Platini.
Kamati ya maadili imeamua kuwasimamisha viongozi hao wa soka wenye ushawishi mkubwa katika mchezo wa soka. Taarifa hizo zimetolewa na mshauri wa zamani wa Blatter akiwa analiambia gaeti la The Guardian kwamba hukumu inasubiriwa kutangazwa wakati wowote.
Blatter ambaye ni raia wa Uswizi amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 1998 na Platini ambaye anataka kumrithi amekana madai yoyote ya kufanya uovu.
No comments
COMMENT