JURGEN KLOPP HATIMAYE KAFIKA LIVERPOOL
Hatimaye mambo yameshakuwa mazuri kwa Jurgen Klopp na hivi sasa ameshatua Liverpool tayari kwa ajili ya kukamilisha mambo ya awali na kutangazwa kesho kama kocha mpya.
Klopp amepigwa picha akiwa kwenye uwanja wa ndege Merseyside akiwasili kwenye ndege binafsi. Kocha huyo raia wa Ujerumani inasemekana atalipwa mshahara wa kiasi cha £4million kwa msimu.
No comments
COMMENT