WELBEK KUWA NJE MPAKA DISEMBA


Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti . Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni. Welbeck, aliumia Goti lake mwezi Aprili huku akiwa kaifungi timu yake ya Arsenal mabao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United. Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji . Dirisha la usajili la kiangazi lilifungwa jumanne iliyopita. Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.