WAKIMBIZI 12,000 WAINGIA UJERUMANI
Utawala mjini Munich kusini mwa Ujerumani unasema kuwa huenda ukakumbwa na changamoto za kuwachukua wakimbizi na wahamiaji zaidi.
Jana Jumamosi watu 13,000 waliwasili mjini humo na sasa nafasi inaripotiwa kuzidi kuwa ndogo .
Meya wa mji huo amesema kuwa uliokuwa uwanja wa olimpiki huenda ukatumika kuwapa hifadhi wakimbizi hao.
Watu wanaingia nchini Ujerumani wakipitia Austria na Hungary ambayo nayo ilishuhudia wakimbizi wengi zaidi jana jumamosi
Serikali ya Hungary inasema kuwa itafunga mpaka na Serbia siku chache zijazo na kuanza kuwakamata wale inaowaita wahamiaji haramu.
No comments
COMMENT