PENATI HAZINA MWENYEWE HATA SISI TUNGESHINDA
Baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kauzu FC nahodha wa Friends Rangers Dan Jeremia amesema, inapofikia hatua ya matuta kila timu inakuwa na nafasi ya kushinda au kushindwa, wao walishindwa lakini walikuwa na nafasi ya kushinda kwenye mikwaju hiyo ya penati.
“Tumefungwa kwenye mchezo wetu wa leo(jana) japo tulicheza vizuri, lakini hatukuweza kupata goli mapema na kulazimika kuingia kwenye hatua ya matuta”, amesema nahodha wa Friends Rangers wakati akihojiwa na kituo cha Azam tv mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Kauzu FC.
“Penati hazina mwenye, timu yoyote inanafasi ya kushinda au kupoteza kwenye hatua hiyo. Wenzetu wameshinda na sisi tumepoteza, huo ndio mpira na tunayaheshimu matokeo. Tunajipanga kucheza mshindi wa tatu na baadae tutaelekea kwenye michuano ya ligi daraja la kwanza”.
“Michuano hii imetusaidia sana katika maandalizi yetu kuelekea ligi daraja la kwanza, Mungu akipenda tutashiriki tena msimu ujao”.
Friends Rangers itacheza dhidi yaMakumba FC siku ya Ijumaa kutafuta mshindi wa tatu wa Ndondo Cup 2015
No comments
COMMENT