JULIO KIBARUA KIPO HATARI

Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo 'Julio'
Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
Kikosi cha wachimba madini cha Mwadui FC leo kinasafiri kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya kuwakabili ‘wagosi wa kaya’ Coastal Union siku ya Juamamosi katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ambayo imeanza kwa kasi msimu huu ikishirikisha timu 16.
Akizungumza na ERICK FELINO kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema kikosi chake kipo kwenye hali nzuri na kwamba safari ya kuelekea Tanga ni kuzifuata pointi tatu.
“Juzi mwalimu wa Toto Africa John Tegete alinipigia simu usiku kunitahadharisha kwamba tusiingie kwenye vyumba kwasababu kuna matatizo. Mimi nashangaa mchezo huo Tanga umeanza lini, wakati mimi niko Tanga kuinusuru Coastal nimecheza miaka yote sijawahi kuona Coastal wanafanya kitu kama hicho na kama watakuwa wanafanya sasahivi watakuwa wanafanya jambo la ajabu”, amesema Julio.
“Tumeondoka leo saa 10 alfajiri kulekea Tanga, timu yetu iko vizuri tunajua kabisa ligi ni ngumu na tulianza kwa kipigo kwenye mechi yetu ya kwanza ugenini, tukashinda kwetu na tukafungwa tena kwetu”.
“Kwahiyo tunafahamu kabisa kila mtu anahitaji kushinda na ninachoshukuru sasahivi waamuzi wamekuwa vizuri sana, ukifanya makosa utafungwa na ukicheza vizuri utashinda na hii yote ni jitihada za TFF chini ya Rais Jamal Malinzi

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.