HATIMA YA KOCHA WA STAND IMETOLEWA

Kocha mkuu wa Stand United Patrick Liewig
Kocha mkuu wa Stand United Patrick Liewig
Baada ya taarifa kuzagaa kuwa benchi la ufundi la timu ya Stand United ‘Chama la wana’ limevunjwa ambalo lipo chini ya mfaransa Patrick Liewig, afisa habari wa timu hiyo Deokaji Makomba ameiuka na kukanusha vikali taarifa hizo akiita ni uvumi.
“Mimi nikwambie hakuna taarifa inayozungumza kuwa benchi la ufundi linavunjwa, benchi la ufundi liko palepale chini ya kocha Patrick Liewig na akishirikiana na Athumani Bilal ‘Bilo’, Mathias Lule kasafiri kidogo kaenda kwao Uganda kwa siku kadhaa lakini baadae atarudi tutakuwa nae” amesema Makomba.
“Benchi letu la ufundi halijavunjwa, tunaliamini kupoteza mechi mbili ni hali ya mchezo kwasababu wewe unajipanga hivi mwenzako anajipanga vile anachukua pointi kwahiyo tuko vizuri tunaendelea kujiandaa ili kuwa bora katika ligi ya Vodacom”.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.