VITU VITATU MUHIMU ANAVYOVIFANYA NIKI WA PILI KABLA YA KUTOA WIMBO MPYA
Rapper kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ametaja vigezo vitatu anavyozingatia kabla ya kutoa wimbo mpya.
Nikki ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Quality Time’ aliyomshirikisha G Nako, ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa kutoa wimbo hadi pale atakaousikiliza na kuridhika yeye binafsi, pia ukipitiwe na member wenzake wa Weusi na watu wake wa kawaida.
“Kabla ya kutoa ngoma mpya kiukweli huwa inaanza na mimi mwenyewe, kuna namna fulani nikiusikiliza kwenye akili yangu kuna kitu fulani kinapita kwenye akili yangu inaniambia huu wimbo ni mkali, halafu nitawashirikisha timu yangu ya Weusi,” amesema Nikki na kuongeza.
“Lakini pia huwa nawasikilizisha watu wa kawaida kabisa kwa sababu mwisho wa siku wao ndio mashabiki, naangalia wao wameupokeaje au wameutafsiri vipo huo wimbo. So nitabalance nikiona mimi mwenye nimeukubali sana, Weusi pia wameukubali sana na watu kadhaa ambao nimewashirikisha ina maana huo wimbo upo katika nafasi kubwa ya kuutoa,” amesisitiza.
No comments
COMMENT