OKWI ATUPIA 4, SIMBA SC RUVU SHOOTING
Mabingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Ngao ya Jamii, Simba SC imechomoza na ushindi mnono wa mabao 7-0 mbele ya Ruvu Shooting mchezo uliyopigwa katika dimba la Uwanja wa Uhuru.
Katika mchezo huo Simba ilitakata katika dakika 45 za kipindi cha kwanza na kupelekea kuchomoza na mabao 5-0 katika kipindi hicho ambapo mchezaji kipenzi cha mashabiki wa wekundu wa msimbazi Simba mganda Emmanuel Arnold Okwi akionyesha maajabu ya kucheka na nyavu.
Magoli ya Simba yamefungwa na Emanuel Okwi katika dakika ya 21 , 22 na 35 wakati bao la nne likifungwa na Shiza Ramadhani Kichuya kunako dakika ya 42 ya mchezo wakati la mwisho ambalo ni la tano katika kipindi cha kwanza likifungwa na mchezaji Juma Liuzio kunako dadika ya 46 kabla ya muamuzi kupiga kipyenga kuashiria mapumziko.
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo wekundu wa msimbazi Simba SC ikajipatia mabao mawili yaliyofungwa na mchezaji wao Okwi pamoja na Erasto Nyoni hivyo kuufanya mchezo huo kumalizika kwa jumla ya mabao 7-0.
No comments
COMMENT