"NIBORA KUWA NA MPENZI BORA NA SIO BORA MPENZI"--Niki wa Pili
Akiwa miongoni mwa wasanii wa HipHop wanaopenda kutoa ushauri na mawaidha kwenye mtandao wa Ig na Twitter, leo Nikki Wa Pili ameandika haya mambo machache kuhusu kuwa MPENZI BORA.
“Ukitaka kuwa mpenzi bora, kuwa mwalimu kwa mwenza wako, mfundishe kila kitu kuhusu wewe nini hupendi, una ndoto gani, ukihuzunika unakuwaje, mabaya na mapungufu yako ni yapi, Usitake mwenza wako awe mganga au mtabiri wa nyota, Yani akujuwe tu bila wewe kumweleza utaishia kusema huyu mwanamke au huyu mwanaume hanielewi kabisa, Achana na movie au nyimbo., Namna pekee ya kueleweka ni kujieleza…….#Jieleze“ alisema Nikki Wa Pili
No comments
COMMENT