DAYNA AOFIA KUDHURUMIWA TUZO YAKE NIGERIA

Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amefunguka kutokabidhiwa tuzo zake mbili alizoshinda katika BEA Awards, 2017 ambazo hutolewa nchini Nigeria.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Chovya’, amesema alishafanya mchakato wa kupata tuzo hizo kipindi cha nyuma lakini hakufanikiwa na kuna kazi zimekuja kumtinga, hivyo kusitisha kufanya hivyo lakini ni kitu ambacho anatamani kukipata.
“Sijapatiwa hadi leo process zao za kutuma sijajua zimekuwaje, imekuwa na uzito wa ugumu nimejaribu kuongea nao mara kwa mara wakaniambia kuna mtu alikuwa atume halafu ikatokea dharura akawa amesafiri akawa amechelewa kurudi na mimi nikawa bize, kwa nikajikuta kila ikitakiwa hivi kuna kuwa na kona kona nyingi au niseme ni mitihani imekuwa mingi japo bado nawasiliana nao, kwa hiyo hazijanifiki,” ameiambia Bongo5.
“Ni kitu ambacho nakitamani kwa sababu ni tuzo zangu za kwanza kupata nje ya Tanzania. Ninaamini tuzo za BEA zimeniongezea kitu kwenye muziki wangu, zinazidi kunikuza na hata kuwepo tena kwenye Afrimma inanifanya nisishtuke,” amesema Dayna.
April 5 mwaka huu Dayna alitangazwa na BEA kushinda katika kipengele cha Best African Artist pamoja na Best Vocal Performance Female.

YouTube

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.