RAPA TYGA ADAIWA DENI KUBWA POLISI WAMTAFUTA
Rb ya rapa Tyga imetolewa na jaji baada ya msanii huyu kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili juu ya kodi ya pango aliyokimbia kulipa.
Aliyekuwa mwenye nyumba wa Tyga anamdai rapa huyu dola $480,000 za nyumba aliyoishi huko Malibu. Mwenye nyumba huyu anataka kujua mali za Tyga zilipo ili akazikusanye na kuzipiga mnada mpaka apate pesa yake.
Mwenye nyumba huyo alikasirishwa na kitendo cha Tyga kununua gari mpya kwaajili ya mpenzi wake iliyogharimu dola $200,000. Kwa sasa Tyga anaishi kwenye nyumba anayolipa dola laki nne na nusu
No comments
COMMENT