MZIGO MPYA WA VIDEO YA DRAKE YADONDOKA KITAANI
Drake kwenye headlines za burudani… baada ya kuachia single yake ya “Hotline Bling”wasanii wengi wa muziki Marekani wamekuwa wakionyesha support yao juu ya single hiyo kwa kufanya remix tofauti ya single hiyo.
Kama wewe ni shabiki mkubwa wa Drake basi ichukue hii mtu wangu, official music video ya “Hotline Bling” imetoka na kama ulikuwa hujui basi ikufikie kuwa wimbo huu kwa sasa unashikilia nafasi ya 2 kwenye chati za Billboard Hot 100 lakini Drake mwenyewe anatamani wimbo huu uguse nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard Hot 100!
Kwenye page yake ya Instagram Drake aliandika…
>>> ” Sijawahi kuwa na namba 1 kwenye chati za Billboard… nahisi ikitokea single yangu ikagusa nafasi ya kwanza mwezi huu wa October itakuwa ni kitu kikubwa sana kwenye kazi yangu ya muziki mpaka sasa…na kama utanitafuta usiku huo nahisi nitakuwa nipo sehemu nimezimia…” <<< @champagnepapi.
Kama bado hujakutana na video ya Hotline Bling, basi feel free kuicheki video hiyo hapa chini.
No comments
COMMENT