JAKAYA AIAGA RASMI IKULU ,LOWASA MAGUFULI AHADI LUKUKI
Ni Jumanne 20 October 2015 na kama kawaida lazima asubuhi ianze na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM. Ninazo zote kubwa za leo kwenye kuperuzi na kudadis, kama zilikupita unaweza ukacheki na hizi nyingine kufidia.
Rais Jakaya Kikwete ameiaga Ikulu na watumishi wake, asema miaka 10 ya uongozi yanatosha kukamilisha agenda yake ya msingi na haitaji miaka mingi zaidi kukamilisha agenda nyingine kwani Rais ajae atampokea kijiti na kuendelea pale alipoishia, amewataka watumishi wa Ikulu kumuonyehsa Rais ajae ushirikiano mkubwa na wakutosha kukamilisha agenda nyingine za maendeleo ya nchi.
Viongozi wa dini wasihi amani juu ya Uchaguzi Mkuu October 25, wamewomba Watanzania kupinga dalili zote zinazoashiria vurugu ya amani pia wamewataka viongozi wa Serikali pamoja na NEC kuhakikisha hatua zote za ulinzi wa amani zinachukuliwa ili kuepusha vurugu zozote zile zinazoweza kutokea.
Mgombea Urais CCM Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein asema kuwa akipata nafasi ya kuwa Rais ataigeuza Zanzibar kuwa kama miji mikubwa ya dunia kama Dubai kwa miradi mbalimbali, Mgombea Urais CCM Tanzania bara, Dk. John Magufuli amewataka Watanzania kukiamini chama cha CCM kwani kimejengwa kwenye misingi ya amani na ahadi zote anzozitoa atahakikisha anazitekeleza kikamilifu ndani ya uongozi wake… mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa ameahidi kutokomeza tatizo la foleni Tunduma ndani ya siku 20 ikiwa akipata ridhaa ya kuongoza nchi kwa awanu ya Serikali ya tano.
Kesi ya mita 200 kuanza leo, jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam leo kuanza kusikiliza kesi ya Kikatiba kuhusu Sheria ya haki ya mpiga kura kukaa umbali wa mita 200 kama ni sahihi au sio sahihi… Rais Jakaya Kikweteamemteua Dk. Katarina Revocatti kuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania naJohn Kayoza kuwa msajiri wa Mahakama ya Rufan
No comments
COMMENT