MOURINHO AMEINGIA KWENYE HEADLINES KWENYE MAGAZETI YA UINGEREZA

Bado mashabiki na wapenzi wa soka duniani kote wanajadili juu ya mwenendo wa klabu ya Chelsea kama Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu UingerezaChelsea ambayo inafundishwa na Jose Mourinho kwa awamu ya pili sasa imekuwa haipati matokeo mazuri kwa siku za hivi karibuni na kwa sasa ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi huku ikiwa na point 11.
Kufuatia mwenendo mbovu wa timu hiyo stori kutoka katika magazeti ya Uingereza ya leo October 26 yanaeleza kuwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich huenda akamfuta kazi Jose Mourinho kwa mara ya pili kama timu ya Chelsea ambayo itacheza mechi naLiverpool katika uwanja wake wa nyumbani Jumamosi ya October 31 itafungwa.
Mourinho-Lampard-City-513573
Taarifa kutoka katika vyombo vingi vya habari Uingereza zinasema kamaChelsea itafungwa na Liverpool Stamford Bridge basi mmiliki wa klabu ya ChelseaRoman Abramovich atamfuta kazi Jose Mourinho, kama Mourinho akifukuzwaChelsea itakuwa ni mara ya pili kufukuzwa kazi baada ya kufukuzwa kwa mara ya kwanza 2007 na kurejea 2013. Nafasi ya Mourinho Chelsea inatajwa kuchukuliwa na Carlo Ancelotti au Guus Hiddink

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.