MCHEZAJI WA SIMBA AKAMATWA NA IRIZI UWANJANI JANA KWENYE MECHI YA SIMBA DHIDI YA PRISO

fvfdghj
Mshambuliaji wa club ya Simba SC, Pape N’daw ametoa kali ya mwaka baada ya kugundulika ana bonge la hirizi katikati ya mechi. N’daw amekutwa akiwa na hirizi kubwa iliyowashtua wachezaji wa Prisons wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara inaendelea kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Wakati mechi inaendelea, mabeki wa Prisons walianzisha tafrani kubwa wakidai N’daw ana hirizi tena ni kubwa kuzidi hata ngumi yake.Hali hiyo ilizua mzozo mkubwa uwanjani hapo, baadaye wachezaji hao walivuta jezi yake na kugundua kweli alikuwa na hirizi.

Baada ya wachezaji wa Simba kuona kweli N’daw alikuwa na hirizi, walishindwa kumtetea na kumuacha mwamuzi achukue uamuzi. 
Mwamuzi wa mchezo huo aliamua kumtoa nje N’daw ili akashushe ‘mzigo’ wake huo na baadaye kurudi uwanjani. 
Mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza kwa N’daw kuanza katika kikosi cha kwanza (11 bora). Lakini ameshindwa kuonyesha uwezo kisoka

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.