MARTIAL ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI LIGI KUU ENGLAND
Klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa miaka miwili sasa ilikuwa haijawahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa sasa imechukuliwa na Anthony Martial mshambuliaji mwenye umri mdogo ambaye aliweka rekodi ya kuuzwa kwa gharama ya juu katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August.
Anthony Martial anakuwa mshambuliaji wa kwanza wa Man United kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi kwani mara ya mwisho mchezaji wa Man United kutwaa tuzo hiyo kabla ya Anthony Martial alikuwa ni Robin van Persie ambaye alitwaa tuzo hiyo mwezi April 2013.
Mshambuliaji huyo kinda wa kifaransa alijiunga na Man United katika dirisha la usajili la majira ya joto 2015 akitokea AS Monaco ya Ufaransa kwa dau la uhamisho wa pound milioni 36, hivyo October 16 ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Man United kutwaa tuzo hiyo katika kipindi cha miaka miwili. Hata hivyo kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi.
No comments
COMMENT