YANGA YASHINDA GEMU YA PILI
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga, imeendelea kufanya kweli kwenye uwanja wa Taifa baada ya jioni ya leo kuibugiza JKT Ruvu jumla ya goli 4-1 kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya ligi hiyo iliyoendelea leo.
Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na mshambuliaji Donald Ngoma katiaka kipindi cha kwanza dakika ya 33 huku goli hilo lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wamecharuka kwani dakika ya 48 kipindi cha pili Amis Tambwe aliifungia Yanga bao la pili, dakikambili baadae Naftali Nashon akaifungia JKT Ruvu goli ambalo liliipa nguvu timu hiyo na kuanza kutafuta goli la kusawazisha.
Wakati JKT Ruvu wakiwa kwenye harakati za kutafuta goli la pili la kusawazisha, Amis Tambwe akapachika goli la tatu dakika ya 60 kwa upande wa Yanga ambalo ni goli lake la pili kwenye mechi ya leo huku Thabani Kamusoko akihitimisha kalamu ya magoli kwa upande wa Yanga kwa kufunga goli la nne dakika ya 87 ya mchezo.
Kikosi cha Yanga kilichoanza: Ally Mustafa, Haji Mwinyi, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela, Amis Tambwe, Donald Ngoma/Malimi Busungu na Deus Kaseke/Geofrey Mwashiuya.
Walioanzina benchi: Deogratius Munish, Salum Telela, Andrey Coutinho, Vicent Bossou, Pato Ngonyani, Malimi Busungu na Geofrey Mwashiuya.
Kikosi cha JKT Ruvu kilichoanza: Tony Kavishe, Michael Aidan, Napho Zuber, Martin Kazila, Madenge Ramadhan, George Minja, Naftali Nashoni, Ismail Aziz /Abdulahman Musa, Samwel Kamuntu/Gaudence Mwaikimba, Saady Kipanga/Emanuel Pius na Mussa Juma.
Walioanzia kwenye benchi:
Shabani Dihile, Issa Ngao, Jaffary Kissoky, Nurdin Mohamed, Emanuel Pius, Abdulahman Musa na Gaudence Mwaikimba.
No comments
COMMENT