WAHAMIAJI WARUHUSIWA KUVUKA CROTIA
Waziri mkuu wa Croatia amesema nchi yake haiwezi kuwazuia wahamiaji wanaotaka kuelekea upande wa magharibi mwa Ulaya.
Zoran Milanovic amesema Croatia itajaribu kuwaandikisha wakimbizi wengine zaidi kadiri itakavyowezekana.
Mamlaka nchini humo zinasema wahamiaji 11,000 wameingia nchini humo baada ya Hungary kufunga mpaka wake wakifunga njia ya kuelekea nchi za EU.
Vurugu zilijitokeza katika eneo la mpaka na Serbia baada ya watu kuchukizwa na hali ya kusubiri kwa muda mrefu.
Makundi ya watu walivuka vizuizi vya watu Tovarnik na Batina huku maelfu ya watu wakingoja usafiri kutoka eneo la mpaka
Waziri wa mambo ya ndani wa Croatia amesema ''nchi imejaa kabisa''
No comments
COMMENT