CHILE YATANGAZA HALI YA DHARURA
Serikali ya Chile imetangaza hali ya dharura katika mji uliokumbwa na tetemeko lenye nguvu.
Watu milioni moja walitakiwa kuacha makazi yao na takriban watu 11 walipoteza maisha baada ya tetemeko lenye ukubwa wa kipimo cha ritcha 8.3 kupiga Jumatano usiku.
Mji wa pwani, Coquimbo, mawimbi ya futi 15 yalipiga pwani. Mawimbi madogo ya Tsunami yalipiga mpaka Alaska.
Rais Michelle Bachelet alitembea Coquimbo Alhamisi.
Tetemeko hili ambalo ndilo kubwa zaidi duniani mwaka huu lilidumu dakika tatu.
Gloria Navarro anayeishi pwani ya mji wa La Serena amesema watu walikuwa wakikimbia ovyo.
Nchini Chile wakazi walionekana wakifanya usafi siku ya Alhamisi baada ya tetemeko linaloelezwa kuwa la sita lenye nguvu.
Kijiji cha Tongoy kiliharibiwa, na zaidi ya nyumba 500 ziliharibiwa vibaya, vikosi vya kupambana na dharura vimeeleza.
Takriban nyumba 90,000 hazina umeme.
No comments
COMMENT