VITU USIVYO VIJUA KUHUSIANA NA DABY KALI KATI YA THE BLUZ NA THE UNNERS
Chelsea na Arsenal ni miongoni mwa ‘Dearby’ kali katika jiji la London hasa kutokana na upinzani wa makocha wanaozinoa timu hizi. Mechi iliyopita baina ya timu hizi ‘Babu’ Wenger alikataa kumpa Mourinho mkono jambo ambalo lilizidisha upinzani kwa mechi zijazo.
Baada ya Jose Mourinho kupata ushindi mnono kwenye usiku wa UEFA wiki hii, mashabiki wengi wanamsubiri kwa hamu kubwa Meneja huyu Jumamosi hii pale ambapo anakutana na kocha mkongwe kwa sasa kwenye EPL ‘Mzee’ Arsenal Wenger. Mourinho anaingia uwanjani huku akiwa ameanza kuchunguzwa na FA juu ya kashfa ya kumtolea maneno ya kibaguzi daktari wa Chelsea anayependwa na wengi mwanamama Ever Carneiro.
Kuelekea mchezo huu, leo nimekuwekea dondoo muhimu kuhusu mchezo huu ambao Mourinho anapaswa kushinda ili kurejesha furaha na imani kwa mashabiki wa Chelsea.
Arsenal itasafiri umbali wa kilometa 344 kutoka Emirates stadium hadi Stamford Bridge umbali wa dakika takribani 200 kwa basi ‘Kibongobongo’ umbali huu ni wa kutoka Mwanza hadi Sengerema.
Mechi baina ya timu hizi itapigwa darajani huku ikichezeshwa na mwamuzi Mike Dean ambaye ana umri wa miaka 47. Dean amekuwa akihusishwa na kuipendelea Chelsea katika matukio kadhaa kwa miaka ya hivi karibuni.
Peter Czech anakwenda Darajani kwa mara ya kwanza kama mpinzani wa Chelsea huku akikumbukwa kwa kuitumikia Chelsea takribani misimu 11. Endapo atafanikiwa kucheza atakamilisha mechi yake ya 6 akiwa na uzi wa Arsenal.
Chelsea inaingia kwenye mechi ya Jumamosi huku ikiwa imeshinda mchezo mmoja katika michezo mitano na kuambulia sare moja nyumbani. ‘The Gurners’ wanaingia uwanjani wakiwa wameshinda mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja huku wakiambulia sare mmoja.
Chelsea imefanya ‘Clean sheets’ tano katika mechi saba ilizokutana na Arsenal. Haya yalitokea kipindi ambacho safu ya ulinzi ya Chelsea ilikuwa imara sana chini ya nahodha John Terry, kwa sasa safu hii ni mbovu na tayari imeruhusu magoli 12 tangu kuanza kwa ligi.
Jose Mourinho hajawahi kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye uwanja wa Stamford Bridge akiwa kama Meneja wa Chelsea. Je, Mzee Wenger ataweza kuvunja rekodi ya Mourinho?
Arsenal haijawahi kuifunga Chelsea kwa misimu mitatu sasa kwenye EPL huku ikiwa imefunga magoli 2 katika mechi 6 za ligi ndani ya misimu hii mitatu. Je Mzee Wenger ataweza kuichachafya safu mbovu ya ulinzi ya Chelsea?
Meneja wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger hajawahi kumfunga Jose Mourinho kwenye EPL. Kumbuka ushindi alioupata Wenger kwenye ngao ya hisani ndio ulikuwa ushindi wake wa kwanza tangu aanze kukutana na Mourinho.
No comments
COMMENT