CHELSEA vs ARSENAL NANI ATAKAYE IBUKA MSHINDI

Chelsea-vs-ArsenalLigi kuu soka nchini England inaendelea tena Jumamosi hii katika viwanja mbalimbali huku Stamford Bridge kukiwa na mtanange wa kutokuukosa kati ya Chelsea ya Mourinho na Arsenal ya Arsene Wenger. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 14:45 saa za Afrika Mashariki.
Team News:
Chelsea wataendelea kumkosa golikipa wao namba 1 Thibaut Qourtois ambaye atakaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu baada ya oparesheni ya goti. Willian anaweza kuukosa mchezo huo, wakati Oscar, Radamel Falcao na Pedro wanaweza kurudi dimbani kutokana na hali zao kuonekana zinatengemaa kutoka majeruhi.
Arsenal wao hawana majeruhi mpya katika kikosi cha kwanza huku golikipa Petr Cech akitarajia kurudi langoni baada ya kupumzishwa Jumatano hii katika michuano ya klabu bingwa Ulaya. Mlinzi Per Mertesacker anaweza kurudi kikosini mara baada ya kupona kutoka alipokua akisumbuliwa na homa wakati Wilshere na Danny Welbeck wakiendelea kuugulia majeraha yao.
Tambo za makocha:
MOURINHO: “katika maisha ni muhimu kujiamini ili kufikia mafanikio, lakini katika soka, ukikosa matokeo unaathirika sana. Unaweza kusema haikuathiri, lakini unaathirika. Wakati timu haifanyi vizuri, stori nyingi za drama hutokea, mara Terry na Costa wamegombana, mara Mourinho hampi mkataba Terry na Ivanovic”.
WENGER: “lazima tukumbuke kuwa huu ni mwanzo tu, tumecheza mechi tano hadi sasa, kwangu mimi hii sio mechi kubwa sana ya msimu, kwa kua najua nafasi yangu mwisho wa msimu itategemea nimeshinda mechi ngapi. Sitaki kufuatilia Chelsea wanashika nafasi ya ngapi muda huu kwakua ligi ndio kwanza inaanza”.
Match Facts:
Chelsea hawajafungwa katika michezo saba iliyopita ya ligi dhidi ya Arsenal (W4 D3)
Arsenal hawajafunga goli lolote katika mechi nne za mwisho za ligi dhidi ya Chelsea huku wakipata magoli mawili tu katika michezo saba ya mwisho dhidi ya Chelsea kwenye ligi.
Arsene Wenger alimfunga Jose Mourinho kwa mara ya kwanza katika mchezo wa ngao ya hisani na kuwa ni ushindi wake wa kwanza katika michezo 14 ya mashindano yote waliyokutana (D6 L7)
Eden Hazard alifunga magoli mawili ya mwisho dhidi ya Arsenal katika mchezo wa ligi Stamford Bridge huku yote yakipatikana kipindi cha kwanza kwa njia ya penati.
Jose Mourinho hajawahi poteza mechi mfululizo katika uwanja wa nyumbani, na tayari kaishafungwa magoli 2-1 na Crystal Palace weekend iliyopita.
Theo Walcott amefunga magoli 11 katika michezo 11 iliyopita akianza katika kikosi cha Arsenal.
Arsenal wameshinda mechi zao zote saba za mwisho za ugenini za ligi hadi sasa huku Chelsea wakiwa hawajaruhusu goli dhidi ya Arsenal katika michezo minne ya mwisho ya ligi.
Vikosi tarajiwa:
Chelsea: Begovic, Ivanovic, Azppilicueta, Cahill, Terry, Matic, Fabregas, Pedro, Oscar, Hazard, Costa.
Arsenal: Cech, Monreal, Bellerin, Koscienly, Mertesacker, Coquelin, Carzola, Ozil, Ramsey, Sanchez, Walcott.

No comments

COMMENT

All rights are recieved.. Powered by Blogger.